Utafiti wa PRISM Family sasa unaalika watu walio na watu waliowapoteza au waliotengana na familia zao kushiriki

Video inaeleza Utafiti wa PRISM Family, na pamoja na kualika wakimbizi waliopoteza familia, utafiti sasa unaingiza na wakimbizi waliotengana na familia.

Hadithi ya kila mtu ni muhimu. Tungependa kujumuisha sauti yako na uzoefu wako katika PRISM Family.

Chuo kikuu cha New South Wales, na Shrika la Msalaba Mwekundu Australaia( Australian Red Cross) na Shirika la Msalaba Mwekundu wa Kimataifa(International Committee of the Red Cross) wameungana pamoja kuangaza mwanga kwenye visa(habari) vya wale ambao walipoteana au kutengana na familia. Utafiti wa PRISM Family ni Mradi mpya wa Kutafiti Athari ya Hali ya Familia Zilizotengana na Mtu Aliyepotea (Project Researching the Impact of Separated and Missing Family).

Utafiti huu unahusu nini?

Familia ni muhimu sana katika maisha yetu. Wakati mwanafamilia hayupo, inaweza kuwa changamwoto na kipindi cha utata.

Mradi wa PRISM Family unalenga kujifunza zaidi kuhusu jinsi kuwa na mwanafamilia aliyepotea kunavyoathiri mawazo, matendo, hisia na ustawi wa mtu. Tungependa pia kujifunza zaidi kuhusu njia mbalimbali ambazo watu wanatumia kukabiliana na kupoteza au kutengana na mwanafamilia na aina ya usaidizi unaofaa zaidi. Utafiti huu utaonyesha uzoefu wa pamoja wa familia zenye wapendwa waliopotea au waliotengana nao.

Pamoja na msaada wako, maarifa kutoka kwa mradi wa PRISM Family utasaidia familia zingine zenye wanafamilia waliopotea au kutengana kupata msaada sahihi na wakati sahihi na kutoa maelezo mapya muhimu ambayo yatatumiwa kutetea mahitaji ya watu waliopotea na familia zao kote ulimwenguni.

Nitaombwa kufanya nini?

Ikiwa unaamua kushiriki, utaombwa kukamilisha maswali kadhaa kwenye kompyuta au simu mahiri yenye ufikiaji wa mtandao katika lugha unayopendelea. Majibu yako yatatunzwa kwa siri  na hayatashirikishwa na mtu mwingine yeyote.

Utafiti wa PRISM Family ni tofauti na tafiti nyingine. Hadithi yako inapoendelea kuchukuliwa, tunataka kuendelea kusikia kutoka kwako. Hii inamaanisha utaombwa kukamilisha utafiti huu mara 4 kwa miaka kama 2.5 (kila miezi 6 hadi mwaka 1).

Kila wakati unapokamilisha uchunguzi utapokea vocha ya ununuzi wa kielektroniki ya $25 Coles kama shukrani.

Usaidizi wa ziada unapatikana kwako na kwa familia yako:

·         Ikiwa huna ufikiaji wa kompyuta au simu mahiri

·         Ikiwa hujawahi kamwe kutumia kompyuta au simu mahiri

·         Ikiwa unahitaji usaidizi wa lugha

Tujulishe kama unahitaji usaidizi wowote wa ziada wakati unapoandikisha nia yako kushiriki katika utafiti huu.

Hakuna shida kama ukiamua kutoshiriki. Unaweza pia kubadilisha mawazo yako na kuamua kuacha kushiriki wakati wowote.

Ikiwa wewe ni mteja wa mradi wa Msalaba Mwekundu wa Australia - Kurejesha Mahusiano ya Familia.

Ikiwa utachagua kushiriki au la, haitabadili jinsi shirika la Msalaba Mwekundu Australia (Australian Red Cross) linavyokusaidia na kuendelea kutafuta majibu kama una mwanafamilia aliyepotea. Uamuzi wetu hautaathiri uhusiano wako na programu ya Australian Red Cross Restoring Family Links, International Committee of the Red Cross, University of New South Wales, au shirika lingine lolote.

 

Je, nitawezaje kuhusika?

Ikiwa unatamani kushiriki katika mradi wa PRISM Family, tafadhali bofya hapa chini na jibu maswali machache. Mara baada ya kumaliza kujaza fomu hii fupi, tutakutumia maelezo zaidi jinsi ya kushiriki katika mradi wa PRISM Family.

Ikiwa wewe au mwanafamilia wako anapendelea kuzungumza na mtu, unaweza kutupigia simu kwenye (02) 9385-0006. Ikiwa unahitaji mkalimani, tujulishe lugha unayopendelea na tutakupigia simu tena tukipata mkalimani.

Unaweza pia kututumia barua pepe moja kwa moja kwenye prism@unsw.edu.au. Ndipo tutakupiga simu tena tukipata mkalimani kama ukihitaji.

 

Wakaribishe Wanafamilia wako

Wanafamilia wengine wa kwako wanaoishi nchini Australia ambao wamepoteana au wametengana na mtu wa familia zao wanaweza pia kushiriki katika utafiti huu. Ikiwa ungetaka kumjulisha mwanafamilia juu ya utafiti huu, unaweza kuingiza anwani yake ya barua pepe na lugha anayopendelea hapa chini. Atatumiwa barua pepe na maelezo kuhusu utafiti huu, na anaweza kuamua kama angetaka kushiriki. Hatutahifadhi habari unazoingiza hapa.